Uimarishwaji Wa Umaizi Mseto Kupitia Mikakati Shirikishi Ya Ufundishaji Wa Kiswahili Nchini Kenya
| dc.contributor.author | Khalili, Ombito E. | |
| dc.date.accessioned | 2018-10-19T06:32:37Z | |
| dc.date.available | 2018-10-19T06:32:37Z | |
| dc.date.issued | 2018-04 | |
| dc.description.abstract | Upataji wa elimu na maarifa ni shughuli isiyo na kikomo katika maisha ya mwanadamu. Ili kuimarisha shughuli hii, lengo la nne la Maendeleo Endelevu linamhitaji kila mwanafunzi kutoachwa nyuma kwenye ujifunzaji na upataji wa maarifa. Lugha ni chombo muhimu katika ufundishaji na ujifunzaji wa somo lolote lile. Hivyo basi, ipo haja ya kumwelekeza mwanafunzi kufikia viwango toshelevu vya umilisi wa lugha, kama chombo cha kujipatia elimu na maarifa ya kudumu maishani. Nadharia ya umaizi mseto, iliyoasisiwa na Howard Gardner inatambua kuwepo kwa aina tofautitofauti za vipawa katika kikundi cha wanafunzi. Vipawa hivi vinastahili kupaliliwa na kukuzwa kwa kutumia mikakati tofautitofauti inayomshirikisha kila mwanafunzi. Naye Lev Vygotsky anapendekeza kutumika kwa mfululizo wa mikakati ya kumwimarisha kila mwanafunzi ili afikie kilele cha matamanio yake kielimu. Ili kuchochea ukuaji wa vipawa na kumshirikisha kila mwanafunzi kwenye somo, mwalimu analazimika kuteuwa na kutumia mikakati kadha anapofundisha. Makala haya yanatathmini mbinu, mikakati na nyenzo shirikishi zinazofaa kutumika katika ufundishwaji wa Kiswahili kwa lengo la kukuza kipawa cha kila mwanafunzi darasani. Mikakati yenyewe inajadiliwa kwa kuangazia utekelezwaji wa mtaala mpya wa elimu nchini Kenya, unaopendekezwa kutumika kuanzia mwaka 2019. Mjadala kwenye makala haya unalenga kujenga uhusiano kati ya nadharia na utekelezwaji wake kwenye shughuli za ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili kama wenzo wa kutimiza malengo ya kitaifa na ya kimataifa kuhusu elimu. Maneno muhimu: ufundishaji, mikakati shirikishi, umaizi mseto. | en_US |
| dc.identifier.isbn | 978-9966-117-37-3 | |
| dc.identifier.uri | http://ir.mksu.ac.ke/handle/123456780/718 | |
| dc.language.iso | en | en_US |
| dc.publisher | Machakos University | en_US |
| dc.subject | Ufundishaji | en_US |
| dc.subject | Mikakati shirikishi | en_US |
| dc.title | Uimarishwaji Wa Umaizi Mseto Kupitia Mikakati Shirikishi Ya Ufundishaji Wa Kiswahili Nchini Kenya | en_US |
| dc.type | Learning Object | en_US |
Files
Original bundle
1 - 1 of 1
Loading...
- Name:
- Uimarishwaji Wa Umaizi Mseto Kupitia Mikakati Shirikishi Ya Ufundishaji Wa Kiswahili Nchini Kenya.pdf
- Size:
- 185.6 KB
- Format:
- Adobe Portable Document Format
- Description:
- Full Text
License bundle
1 - 1 of 1
Loading...
- Name:
- license.txt
- Size:
- 1.71 KB
- Format:
- Item-specific license agreed upon to submission
- Description:
