USAWIRI WA WAHUSIKA WA KIUME KATIKA RIWAYA ZA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI
| dc.contributor.author | KIEMA AGNES MWONGELI | |
| dc.date.accessioned | 2025-11-13T06:07:46Z | |
| dc.date.available | 2025-11-13T06:07:46Z | |
| dc.date.issued | 2025-11 | |
| dc.description.abstract | Katika karne ya ishirini na moja, mwanamke amewekwa mbele kinyume na ilivyokuwa wakati dunia ilikuwa imetawaliwa na ubabedume. Hali hii inasawiri mabadiliko katika jamii. Mabadiliko haya yamemwathiri mwanamume katika jamii. Utafiti huu ulichunguza usawiri wa wahusika wa kiume katika riwaya ya Chozi la Heri na Nguu za Jadi. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uhalisia. Nadharia ya uhalisia inadai kwamba, fasihi inalenga kutoa picha halisi ya jamii husika. Nadharia hii ilizuka huko Ulaya katika karne ya kumi na tisa. Miongoni mwa wataalamu waliohusishwa na nadharia hii ni Georg Lukacs (1972). Utafiti huu ulilenga kuchunguza jinsi mhusika wa kiume anavyosawiriwa katika riwaya teule. Aidha, umebainisha changamoto zinazomkabili mhusika wa kiume katika riwaya teule. Halikadhalika, utafiti huu umeonyesha jinsi changamoto zinazomkabili mhusika wa kiume zinavyomwathiri binafsi na jamii yake. Utafiti huu ulikuwa wa maktabani ambapo riwaya ya Chozi la Heri na Nguu za Jadi zilisomwa na kuhakikiwa. Riwaya hizi zilichanguliwa kimakusudi. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa na kuwasilishwa kimaelezo. Utafiti huu umeangazia masuala ya jinsia ya kiume, jambo ambalo linahusu jamii kwa jumla. Vilevile, kutokana na utafiti huu, jamii itaweza kubaini changamoto mbalimbali zinazoikabili jinsia ya kiume na athari ya changamoto hizo na hivyo, kuwa na uwezo wa kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo. Halikadhalika, utafiti huu utakuwa kichocheo na rejea muhimu kwa watafiti wa baadaye wa fasihi kuchunguza masuala yanayohusu jinsia ya kiume. | en_US |
| dc.identifier.uri | http://ir.mksu.ac.ke/handle/123456780/20020 | |
| dc.language.iso | en | en_US |
| dc.publisher | Machakos University Press | en_US |
| dc.title | USAWIRI WA WAHUSIKA WA KIUME KATIKA RIWAYA ZA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI | en_US |
| dc.type | Thesis | en_US |