Server maintenance in progress. Please bear with us

Kiswahili na Maendeleo Mashambani Nchini Kenya

Loading...
Thumbnail Image

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Machakos University

DOI

Abstract

Makala hii itatathmini umuhimu wa lugha (Kiswahili) katika kuchangia maendeleo nchini Kenya. Maendeleo yamejelezwa na wataalamu mbalimbali. Chambers (1997) ameeleza ‘maendeleo’ kwa usahili kabisa kuwa ni ‘mabadiliko mazuri’ (nchini au duniani). Alan Thomas (2000) ameyaeleza kama kuboreka kwa hali ya maisha, afya na maisha bora kwa wote na mafanikio ambayo huleta uzuri wa maisha kwa jamii yote. Haya hutokea kwa awamu ya muda mrefu. Maendeleo kwa jumla humaanisha mabadiliko chanya ya mwanadamu katika harakati zake zote za kimaisha.Maendeleo ni lazima kwa mwanadamu duniani. Hakuna wanadamu wanaobaki kama walivyo miaka nenda miaka rudi. Kuna maendeleo ya kibinafsi na ya kijamii. Yote haya huwezeshwa na kiwango cha uchumi. Uchumi hukua kutokana na uzalishaji mali. Uzalishaji mali hutokea katika mashamba na mitambo au viwanda. Uwezo huu huletwa na jamii kujifunza mbinu na stadi za uzalishaji mali. Mtu anapojifunza stadi fulani, lazima atumie lugha, lugha anayoielewa. Kwa hivyo, stadi haziletwi na Kiingereza bali lugha yoyote ile. Nchi nyingi ulimwenguni hazitumii Kiingereza na zimeendelea sana, mfano Ujarumani, Ufaransa, Italy, Malasyia, Korea Kisini na kadhalika. Kwa hivyo, natujiulize, je, hapa Kenya tunaweza kutumia Kiswahili kujifunza mbinu na stadi mbali mbali za kuzalisha mali? Hii ni kwa sababu Kiswahili ni somo la lazima nchini kutoka shule za msingi hadi shule za sekondari. Aidha ni lugha rasmi na ya taifa. Hivyo ni lingua franca nchini. Katika makala hii ninajaribu kudadisi swala hili na kutoa mifano kadhaa iliyopatikana nchini Kenya. Maneno makuu: maendeleo, uchumi, mawasiliano, lugha, elimu

Description

Keywords

Citation

Endorsement

Review

Supplemented By

Referenced By