• Login
    View Item 
    •   MKSU Digital Repository Home
    • Projects, Theses and Dissertations
    • MKSU Masters Theses
    • MKSU Masters Theses
    • View Item
    •   MKSU Digital Repository Home
    • Projects, Theses and Dissertations
    • MKSU Masters Theses
    • MKSU Masters Theses
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    MCHANGO WA MANDHARI KATIKA KUFANIKISHA UJUMBE KATIKA RIWAYA ROSA MISTIKA NA MAISHA KITENDAWILI

    Thumbnail
    View/Open
    Full Text (1016.Kb)
    Date
    2023-03
    Author
    MUIA, SHADRACK TETE
    Metadata
    Show full item record
    Abstract
    Lengo la kila mwandishi wa kazi ya fasihi ni kufikisha ujumbe kwa msomaji. Ili kuwasilisha ujumbe huo kikamilifu, inambidi mwandishi atumie mbinu za kisanii mbalimbali. Mbinu za kisanii hujumuisha jinsi masimulizi hufanywa kupitia kwa wahusika, mbinu za uandishi, mandhari na lugha. Mandhari ni mojawapo ya kipengele cha mbinu za kisanii ambacho hudokeza mahali matukio ya hadithi au masimulizi hutokea. Kila jambo linalotendeka katika jamii hutendeka mahali fulani na kazi za kifasihi nazo hufanya vivyo hivyo. Mandhari huweza kuwa halisi au ya kidhanifu. Mandhari na ujumbe hutegemeana kwa kuwa mtunzi asiposawiri mandhari vilivyo, ujumbe hauwezi kuwasilishwa kwa msomaji kikamilifu. Kwa mfano anapoeleza ujumbe kuhusu wanyonge, lazima atumie mandhari duni kama vile mitaa ya mabanda. Azma ya utafiti huu ni kuchunguza mchango wa mandhari ifaayo ili kufanikisha ujumbe wa mwandishi katika riwaya mbili za Kiswahili Rosa Mistika (Kezilahabi) na Maisha Kitendawili (Habwe). Riwaya hizi zilichaguliwa kupitia usampuli wa kimakusudi na zimeandikwa na waandishi tofauti, mmoja wa nchi ya Tanzania na mwingine wa Kenya. Pia riwaya hizi ziliandikwa miaka ya 1971 na 2000 mtawalia. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uhalisia. Nadharia ya uhalisia inadai kuwa msanii anatarajiwa kutoa picha za matukio na mazingira halisi ambayo yanaonekana ili kuchora maisha kama yalivyo katika jamii. Kazi hii ilikuwa na malengo haya: kwanza, kubainisha mandhari mbalimbali yaliyochorwa na waandishi. Pili, kuchunguza mchango wa mandhari katika kufanikisha ujumbe wa mwandishi. Mwisho, kutathmini ikiwa mandhari yaliyotumiwa na waandishi yameakisi hali halisi ya jamii. Utafiti huu umekuwa wa maktabani na data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kuzingatia mihimili ya nadharia na matokeo yamewasilishwa kimaelezo. Utafiti uligundua kuwa mandhari ni muhimu sana kwa mwandishi kuwasilisha ujumbe wake kikamilifu. Matumaini ya mtafiti ni kuwa utafiti huu utakuwa na manufaa kwa wahakiki, wasomi na walimu, wakuza mitaala na wanafunzi wa vyuo vikuu. Vilevile utachangia katika taaluma ya uhakiki na fasihi ya Kiswahili kwa jumla.
    URI
    http://ir.mksu.ac.ke/handle/123456780/17617
    Collections
    • MKSU Masters Theses [123]

    DSpace software copyright © 2002-2015  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    @mire NV
     

     

    Browse

    All of Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsBy Submit DateThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsBy Submit Date

    My Account

    LoginRegister

    DSpace software copyright © 2002-2015  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    @mire NV