Show simple item record

dc.contributor.authorMutua, John
dc.contributor.authorChimerah, Rocha
dc.contributor.authorNgowa, Nancy
dc.date.accessioned2019-04-16T08:50:59Z
dc.date.available2019-04-16T08:50:59Z
dc.date.issued2017
dc.identifier.issn2520-0577
dc.identifier.urihttp://ir.mksu.ac.ke/handle/123456780/4300
dc.description.abstractUhusiano kati ya jinsia ya kiume na ya kikeni ni suala linaloendelea kuzua mijadala si haba miongoni mwa jamii kila uchao. Aghalabu midahalo hiyo huibua mitazamo kinzani baina ya wasomi na wahakiki wa kazi za kifasihi. Baadhi ya kazi hizo za kifasihi ni zile zilizohakikiwa kwa misingi ya nadharia ya kifeministi. Tahakiki hizo zimekuwa zikichochea fikira kwamba, waandishi wa kiume ndio wanaopaswa kulaumiwa kwa kuendeleza usawiri usiopendeza kwa wahusika wa kike katika fasihi. Hali hii imevyaza dhana kuwa waandishi wa kiume huwasawiri wahusika wa kike kwa mtazamo tofauti wakilinganishwa na waandishi wa kike. Ikiwa mawazo hayo ni ya kusadikika, basi itakuwa sawa na kudai ya kwamba waandishi wa kike huwasawiri wahusika wa kike kwa mtazamo unaopendeza katika fasihi. Je, waandishi wa kiume husawiri wahusika tofauti na waandishi wa kike? Ili kulijibu swali hili tumelinganisha waandishi wa jinsia tofauti.Kufungamana na mkabala huu wa uwazaji, makala hii imelinganisha waandishi wa jinsia ya kike na ya kiume kwa lengo la kubainisha mitazamo yao kuhusu usawiri wa mhusika wa kike katika tamthilia za Kiswahili. Tumelinganisha tamthilia ya mwandishi wa kike; Mama Ee ya Mwachofi A. (1987) na Posa za Bikisiwa (2003) ya waandishi wa kiume ambao ni; King’ei K. na Mohamed S. Tamthilia ya Posa za Bikisiwa ilichapishwa miongo miwili baada ya Mama Ee na hivyo inadhihirisha mtazamo tofauti wa taswira ya kike ikilinganishwa na Mama Ee. Hata hivyo, mpito wa wakati huenda umechangia mabadiliko katika mitazamo ya kusawiri wahusika wa kike. Pia, inakisiwa kuwa jinsia ya mwandishi inaathiri usawiri huu. Waandishi wa tamthilia hizi waliwapa wahusika wa kike sifa mbalimbali ambazo zinaashiria mitazamo yao. Licha ya kwamba waandishi hao wote wamejadili maudhui sawa, wameonyesha tofauti ya kimtazamo katika masuala ya uongozi, utabaka, ndoa na upotovu wa kimaadili miongoni mwa maudhui mengine. Ili kufikia lengo la makala hii tumeongozwa na nadharia ya ufeministi wa Baada-ukoloni. Nadharia hii imetuwezesha kuchunguza sifa za mwanamke Mwafrika kama alivyosawiriwa na waandishi wa Kiafrika.en_US
dc.language.isoen_USen_US
dc.publisherThe Africa Premier Research Publishing Huben_US
dc.subjectChanya – Inayopendeza, -enye thamani, -enye kustahili au kinyume cha hasi.en_US
dc.subjectMtazamo – Namna kitu, jambo au hali inavyofikiriwa kuwa, hisia alizonazo mtu kuhusu mtu, kitu au hali.en_US
dc.subjectMwanamke – imetumika kurejelea wanawake (wingi).en_US
dc.subjectUfeministi wa Baada-ukoloni – Nadharia ya uhakiki wa fasihi inayohusishwa na mtazamo wa Kiafrikaen_US
dc.titleMitazamo ya Kusawiri Wahusika wa Kike katika Tamthilia za Kiswahili: Posa za Bikisiwa na Mama Eeen_US
dc.typeArticleen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record