• Login
    View Item 
    •   MKSU Digital Repository Home
    • Research and Publications
    • School of Education
    • School of Education
    • School of Education
    • View Item
    •   MKSU Digital Repository Home
    • Research and Publications
    • School of Education
    • School of Education
    • School of Education
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Mitazamo ya Kusawiri Wahusika wa Kike katika Tamthilia za Kiswahili: Posa za Bikisiwa na Mama Ee

    Thumbnail
    View/Open
    Full Text (229.3Kb)
    Date
    2017
    Author
    Mutua, John
    Chimerah, Rocha
    Ngowa, Nancy
    Metadata
    Show full item record
    Abstract
    Uhusiano kati ya jinsia ya kiume na ya kikeni ni suala linaloendelea kuzua mijadala si haba miongoni mwa jamii kila uchao. Aghalabu midahalo hiyo huibua mitazamo kinzani baina ya wasomi na wahakiki wa kazi za kifasihi. Baadhi ya kazi hizo za kifasihi ni zile zilizohakikiwa kwa misingi ya nadharia ya kifeministi. Tahakiki hizo zimekuwa zikichochea fikira kwamba, waandishi wa kiume ndio wanaopaswa kulaumiwa kwa kuendeleza usawiri usiopendeza kwa wahusika wa kike katika fasihi. Hali hii imevyaza dhana kuwa waandishi wa kiume huwasawiri wahusika wa kike kwa mtazamo tofauti wakilinganishwa na waandishi wa kike. Ikiwa mawazo hayo ni ya kusadikika, basi itakuwa sawa na kudai ya kwamba waandishi wa kike huwasawiri wahusika wa kike kwa mtazamo unaopendeza katika fasihi. Je, waandishi wa kiume husawiri wahusika tofauti na waandishi wa kike? Ili kulijibu swali hili tumelinganisha waandishi wa jinsia tofauti.Kufungamana na mkabala huu wa uwazaji, makala hii imelinganisha waandishi wa jinsia ya kike na ya kiume kwa lengo la kubainisha mitazamo yao kuhusu usawiri wa mhusika wa kike katika tamthilia za Kiswahili. Tumelinganisha tamthilia ya mwandishi wa kike; Mama Ee ya Mwachofi A. (1987) na Posa za Bikisiwa (2003) ya waandishi wa kiume ambao ni; King’ei K. na Mohamed S. Tamthilia ya Posa za Bikisiwa ilichapishwa miongo miwili baada ya Mama Ee na hivyo inadhihirisha mtazamo tofauti wa taswira ya kike ikilinganishwa na Mama Ee. Hata hivyo, mpito wa wakati huenda umechangia mabadiliko katika mitazamo ya kusawiri wahusika wa kike. Pia, inakisiwa kuwa jinsia ya mwandishi inaathiri usawiri huu. Waandishi wa tamthilia hizi waliwapa wahusika wa kike sifa mbalimbali ambazo zinaashiria mitazamo yao. Licha ya kwamba waandishi hao wote wamejadili maudhui sawa, wameonyesha tofauti ya kimtazamo katika masuala ya uongozi, utabaka, ndoa na upotovu wa kimaadili miongoni mwa maudhui mengine. Ili kufikia lengo la makala hii tumeongozwa na nadharia ya ufeministi wa Baada-ukoloni. Nadharia hii imetuwezesha kuchunguza sifa za mwanamke Mwafrika kama alivyosawiriwa na waandishi wa Kiafrika.
    URI
    http://ir.mksu.ac.ke/handle/123456780/4300
    Collections
    • School of Education [203]

    DSpace software copyright © 2002-2015  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    @mire NV
     

     

    Browse

    All of Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsBy Submit DateThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsBy Submit Date

    My Account

    LoginRegister

    DSpace software copyright © 2002-2015  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    @mire NV