dc.description.abstract | Tamthilia ya Kiswahili ina historia fupi ikilinganishwa na tanzu zingine, hasa ushairi. Tamthilia za kwanza kuwahi kutafsiriwa kwa Kiswahili na zilizoandikwa kwa lugha hii zilizingatia sana maudhui ya kidini, kizalendo, utetezi dhidi ya dhuluma tawala za kigeni na hasa ukoloni mamboleo. Kinyume na hali hiyo, tamthilia ya Kiswahili katika kipindi cha kuanzia 1950 hadi miaka ya 2000 umesheheni wingi wa tungo zinazosifia Uafrika na heshima ya mtu mweusi hapa barani Afrika na kote ulimwenguni. Uchunguzi wa tamthilia hizi unadhihirisha kujitolea kwa dhati kwa watunzi wake kuelezea, kutetea na kuhimiza heshima ya Mwafrika. Maudhui yake yanakiuka yale masuala finyu ya utaifa, uraia na tawala za mataifa ya Kiafrika. Hii ndio maana makala haya yanalenga kufafanua nadharia na maoni ya wanaujumi mweusi na jinsi fikira zao zilivyoathiri na kuongoza mitazamo ya watunzi wa tamthilia. Data ya makala haya ilikusanywa katika tamthilia ya M a s h e t a n i W a m e r u d i (Mohamed 2016). Tamthilia hii iliteuliwa kwa kutumia mbinu kusudio. Hii ni kwa sababu usomi awali ulionyesha kuwa tamthilia hii imetumia misingi ya nadharia ya ujumi mweusi. Data yenyewe ilikuwa ya kimaelezo na ilichanganuliwa vilevile kwa njia ya maelezo. Makala yalionyesha namna ambavyo mwandishi ameweka wazi hadhi ya Mwafrika na kudhihirisha kuwa amejitambua na anapaswa kutambuliwa na kuheshimiwa na ulimwengu mzima. Hii ni baada ya Mwafrika kuelewa kwamba watu kutoka mabara mengine sio bora kumliko kama ambavyo watu hawa hutaka ichukuliwe na Mwafrika | en_US |