• Login
    View Item 
    •   MKSU Digital Repository Home
    • Conferences / Workshops / Seminars
    • Conferences
    • 2nd International Conference
    • View Item
    •   MKSU Digital Repository Home
    • Conferences / Workshops / Seminars
    • Conferences
    • 2nd International Conference
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Tathmini Ya Ujumi Mweusi Katika Tamthilia Ya Mashetani Wamerudi (S.A.M 2016)

    Thumbnail
    View/Open
    Full Text (2.093Mb)
    Date
    2019-04
    Author
    Muusya, Justus Kyalo
    Metadata
    Show full item record
    Abstract
    Tamthilia ya Kiswahili ina historia fupi ikilinganishwa na tanzu zingine, hasa ushairi. Tamthilia za kwanza kuwahi kutafsiriwa kwa Kiswahili na zilizoandikwa kwa lugha hii zilizingatia sana maudhui ya kidini, kizalendo, utetezi dhidi ya dhuluma tawala za kigeni na hasa ukoloni mamboleo. Kinyume na hali hiyo, tamthilia ya Kiswahili katika kipindi cha kuanzia 1950 hadi miaka ya 2000 umesheheni wingi wa tungo zinazosifia Uafrika na heshima ya mtu mweusi hapa barani Afrika na kote ulimwenguni. Uchunguzi wa tamthilia hizi unadhihirisha kujitolea kwa dhati kwa watunzi wake kuelezea, kutetea na kuhimiza heshima ya Mwafrika. Maudhui yake yanakiuka yale masuala finyu ya utaifa, uraia na tawala za mataifa ya Kiafrika. Hii ndio maana makala haya yanalenga kufafanua nadharia na maoni ya wanaujumi mweusi na jinsi fikira zao zilivyoathiri na kuongoza mitazamo ya watunzi wa tamthilia. Data ya makala haya ilikusanywa katika tamthilia ya M a s h e t a n i W a m e r u d i (Mohamed 2016). Tamthilia hii iliteuliwa kwa kutumia mbinu kusudio. Hii ni kwa sababu usomi awali ulionyesha kuwa tamthilia hii imetumia misingi ya nadharia ya ujumi mweusi. Data yenyewe ilikuwa ya kimaelezo na ilichanganuliwa vilevile kwa njia ya maelezo. Makala yalionyesha namna ambavyo mwandishi ameweka wazi hadhi ya Mwafrika na kudhihirisha kuwa amejitambua na anapaswa kutambuliwa na kuheshimiwa na ulimwengu mzima. Hii ni baada ya Mwafrika kuelewa kwamba watu kutoka mabara mengine sio bora kumliko kama ambavyo watu hawa hutaka ichukuliwe na Mwafrika
    URI
    http://ir.mksu.ac.ke/handle/123456780/4927
    Collections
    • 2nd International Conference [101]

    DSpace software copyright © 2002-2015  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    @mire NV
     

     

    Browse

    All of Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsBy Submit DateThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsBy Submit Date

    My Account

    LoginRegister

    DSpace software copyright © 2002-2015  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    @mire NV