dc.description.abstract | Makala hii itatathmini umuhimu wa lugha (Kiswahili) katika kuchangia maendeleo nchini Kenya.
Maendeleo yamejelezwa na wataalamu mbalimbali. Chambers (1997) ameeleza ‘maendeleo’ kwa
usahili kabisa kuwa ni ‘mabadiliko mazuri’ (nchini au duniani). Alan Thomas (2000) ameyaeleza
kama kuboreka kwa hali ya maisha, afya na maisha bora kwa wote na mafanikio ambayo huleta
uzuri wa maisha kwa jamii yote. Haya hutokea kwa awamu ya muda mrefu. Maendeleo kwa jumla
humaanisha mabadiliko chanya ya mwanadamu katika harakati zake zote za kimaisha.Maendeleo
ni lazima kwa mwanadamu duniani. Hakuna wanadamu wanaobaki kama walivyo miaka nenda
miaka rudi. Kuna maendeleo ya kibinafsi na ya kijamii. Yote haya huwezeshwa na kiwango cha
uchumi. Uchumi hukua kutokana na uzalishaji mali. Uzalishaji mali hutokea katika mashamba na
mitambo au viwanda. Uwezo huu huletwa na jamii kujifunza mbinu na stadi za uzalishaji mali.
Mtu anapojifunza stadi fulani, lazima atumie lugha, lugha anayoielewa. Kwa hivyo, stadi haziletwi
na Kiingereza bali lugha yoyote ile. Nchi nyingi ulimwenguni hazitumii Kiingereza na zimeendelea
sana, mfano Ujarumani, Ufaransa, Italy, Malasyia, Korea Kisini na kadhalika. Kwa hivyo,
natujiulize, je, hapa Kenya tunaweza kutumia Kiswahili kujifunza mbinu na stadi mbali mbali za
kuzalisha mali? Hii ni kwa sababu Kiswahili ni somo la lazima nchini kutoka shule za msingi hadi
shule za sekondari. Aidha ni lugha rasmi na ya taifa. Hivyo ni lingua franca nchini. Katika makala
hii ninajaribu kudadisi swala hili na kutoa mifano kadhaa iliyopatikana nchini Kenya.
Maneno makuu: maendeleo, uchumi, mawasiliano, lugha, elimu | en_US |