Taswira ya Gereza Katika Riwaya ya Haini (Shafi Adam Shafi): Uhakiki wa Ki- Foucault
View/ Open
Date
2018-04Author
Mutua, John M.
Mogere, Gerald O.
Muusya, Justus K.
Metadata
Show full item recordAbstract
IKISIRI
Makala hii inakusudiwa kutalii jinsi gereza ilivyotumiwa kama msingi wa kuendeleza maudhui
katika riwaya ya Haini ya Shafi Adam Shafi. Aidha, inapania kudhihirisha jinsi maudhui ya jamii
ya kigereza yanavyobainika kuambatana na sifa zinazotambuliwa na Michael Foucault ambaye ni
mwasisi wa nadharia ya Ki-Foucault inayoongoza uhakiki huu. Aghalabu msanii wa fasihi
huchota malighafi yake kutokana na jamii anamokulia pamoja na tajriba yake inayoongozwa na
ubunifu wake. Pia, matukio na asasi mbalimbali za jamii hutoa mchango mkubwa katika
kuendeleza maudhui katika fasihi ya Kiswahili. Gereza ni mojawapo ya asasi zinazokuwa
chemichemi ya maudhui yanayoendeleza fasihi katika jamii.Maudhui ni kipengele muhimu katika
kazi ya fasihi, yanapofafanuliwa na kueleweka na msomaji, hapo ndipo lengo la mwandishi
hukamilika. Katika msingi huu tumedhamiria kuchunguza jukumu la mfumo wa kigereza na athari
zake katika jamii kwa kurejerea Haini.