• Login
    View Item 
    •   MKSU Digital Repository Home
    • Conferences / Workshops / Seminars
    • Conferences
    • 1st International Conference
    • View Item
    •   MKSU Digital Repository Home
    • Conferences / Workshops / Seminars
    • Conferences
    • 1st International Conference
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Uimarishwaji Wa Umaizi Mseto Kupitia Mikakati Shirikishi Ya Ufundishaji Wa Kiswahili Nchini Kenya

    Thumbnail
    View/Open
    Full Text (185.6Kb)
    Date
    2018-04
    Author
    Khalili, Ombito E.
    Metadata
    Show full item record
    Abstract
    Upataji wa elimu na maarifa ni shughuli isiyo na kikomo katika maisha ya mwanadamu. Ili kuimarisha shughuli hii, lengo la nne la Maendeleo Endelevu linamhitaji kila mwanafunzi kutoachwa nyuma kwenye ujifunzaji na upataji wa maarifa. Lugha ni chombo muhimu katika ufundishaji na ujifunzaji wa somo lolote lile. Hivyo basi, ipo haja ya kumwelekeza mwanafunzi kufikia viwango toshelevu vya umilisi wa lugha, kama chombo cha kujipatia elimu na maarifa ya kudumu maishani. Nadharia ya umaizi mseto, iliyoasisiwa na Howard Gardner inatambua kuwepo kwa aina tofautitofauti za vipawa katika kikundi cha wanafunzi. Vipawa hivi vinastahili kupaliliwa na kukuzwa kwa kutumia mikakati tofautitofauti inayomshirikisha kila mwanafunzi. Naye Lev Vygotsky anapendekeza kutumika kwa mfululizo wa mikakati ya kumwimarisha kila mwanafunzi ili afikie kilele cha matamanio yake kielimu. Ili kuchochea ukuaji wa vipawa na kumshirikisha kila mwanafunzi kwenye somo, mwalimu analazimika kuteuwa na kutumia mikakati kadha anapofundisha. Makala haya yanatathmini mbinu, mikakati na nyenzo shirikishi zinazofaa kutumika katika ufundishwaji wa Kiswahili kwa lengo la kukuza kipawa cha kila mwanafunzi darasani. Mikakati yenyewe inajadiliwa kwa kuangazia utekelezwaji wa mtaala mpya wa elimu nchini Kenya, unaopendekezwa kutumika kuanzia mwaka 2019. Mjadala kwenye makala haya unalenga kujenga uhusiano kati ya nadharia na utekelezwaji wake kwenye shughuli za ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili kama wenzo wa kutimiza malengo ya kitaifa na ya kimataifa kuhusu elimu. Maneno muhimu: ufundishaji, mikakati shirikishi, umaizi mseto.
    URI
    http://ir.mksu.ac.ke/handle/123456780/718
    Collections
    • 1st International Conference [82]

    DSpace software copyright © 2002-2015  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    @mire NV
     

     

    Browse

    All of Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsBy Submit DateThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsBy Submit Date

    My Account

    LoginRegister

    DSpace software copyright © 2002-2015  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    @mire NV